Featured Post

5 Things to Do to Secure Your Facebook Account From Hackers

Image
  Some time back, a Facebook account was irrelevant to hackers. There was no reason to hack anyone’s account since there was no reason for hacking an account in the first place. Ever since it has grown to billions of users, Facebook contains enough data for hackers to use for either monetary gain or blackmail. A celebrity’s account, for example, can be hacked in order for a person to advertise a page or brand. The hacker can also post embarrassing or discriminating posts that will leave the celeb’s fans furious. Your account is also prone to hacking even if you aren’t a celebrity. You obviously have to protect your  Facebook account from malicious hackers . It is not that hard to protect your account. Just follow these guidelines, and you’ll be good to go: 1) AVOID SAVING PASSWORDS ON PUBLIC DEVICES Cybercafés are awesome alternatives when you do not have any data on your device. They are also reserves for passwords since most people just click on ‘yes’ on the save password di...

Orodha mpya ya matajiri Afrika



Orodha mpya ya mabilionea Afrika yamshirikisha Dangote , Mo Dewji na Isabel dos Santos Abdalla Seif Dzungu BBC Swahili 18 Januari 2020 Aliko Dangote CHANZO CHA PICHA,AFP Maelezo ya picha, Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote Mfanyabiashara Mohammed Dewji kutoka Tanzania ametajwa kuwa miongoni mwa mabilioni 20 wa Afrika katika ripoti ya jarida la Forbes la mwaka 2020. Hatahivyo utajiri wa bilionea wa Tanzania Mo umedaiwa kupungua hadi dola bilioni 1.6. Katika ripoti hiyo mfanyabiashara tajiri nchini Nigeria Aliko Dangote ameorodheshwa kwa mara ya tisa mfululizo, kuwa mtu tajiri zaidi barani Afrika . Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara ya Simiti, Sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1. Pia unaweza kusoma: Vijana walio tajiri zaidi duniani Watu wanane matajiri kupindukia duniani Dangote anafuatiwa na mfanyabiashara wa Misri Nassef Sawaris ambaye aliongeza utajiri wake kutoka dola bilioni 6.3 hadi dola bilioni nane. Mfanyabiashara huyo anamiliki asilimia 5.7 ya hisa za kamapuni ya viatu ya Adidas . Ongezeko la hisa za Adidas liliomuongezea dola bilioni moja nukta tano katika akaunti yake. Mo Dewji CHANZO CHA PICHA,HAKI MILIKI YA PICHAAFP/GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Bilionea kutoka Tanzania Mo Dewji Bilionea aliyeorodheshwa katika nafasi ya tatu ni raia wa Nigeria Mike Adenuga ambaye utajiri wake unatokana na sekta ya mawasiliano na mafuta. Kampuni yake ya mawasiliano ya simu Globacom ndio ya tatu kwa ukubwa nchini Nigeria ikiwa na wateja milioni 43. Alijipatia utajiri wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 26 akiuza kanda za viatu na vinywaji. Bilionea aliyeorodheshwa wa nne barani Afrika ni mfanyabiashara wa almasi na raia wa Afrika Kusini Nicky Oppenheimer. Nicky ambaye ni mrithi wa mali ya familia yake ya Oppenheimer ana utajiri wa dola bilioni 7.7. Familia yake imekuwa ikihusika na uuzaji wa almasi. Isabel dos Santos mwenye utajiri wa dola bilioni 2.2 amedaiwa kujipatia utajiri wake wakati babake alipokuwa rais ambapo alijipatia hisa katika makampuni mengi ya Angola pamoja na benki. Mwanamke huyo ambaye ametajwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika amesema kwamba anamiliki hisa kutoka kampuni zilizopo Ureno, ikiwemo Telecom na runinga ya nyaya. Msemaji wa Isabel aliambia jarida la Forbes kwamba ni mfanyabiashara huru . Isabel dos Santos

Comments

Popular posts from this blog

5 Things to Do to Secure Your Facebook Account From Hackers

10 Things Every Woman Can't Hide When They Are In Love With a Man

If A Man Does These Things, it Means his Love For You Will Never Die