Featured Post
HABARI:Wachawi Waapa Kumroga Aliyechoma Moto Kanisa Lao
- Get link
- X
- Other Apps
MAMBO yaligeuka mnamo Alhamisi, Januari 14, 2021, mnamo saa kumi na moja asubuhi wakati mtu asiyejulikana aliteketeza jumba la “Halloween House” jijini New York, nchini Marekani.
Nyumba hiyo maarufu kama House of Netherworld imejengwa eneo ambalo lilibandikwa jina la Witchcraft District mjini Poughkeepsie. Nyumba hiyo ni mahali patakatifu pa wanachama wa Kanisa la Shetani. Kulingana na ripoti ya polisi, kulikuwa na watu wawili ndani ya nyumba hiyo lakini wote walinusurika kifo.
Katika video ya CCTV, mwanamme mmoja anaonyeshwa akiingia ndani ya nyumba hiyo akiwa amebeba vibuyu vya mafuta ambapo alimwagilia majengo hayo kabla ya kuwasha moto na kisha kutoroka huku akikosa kujulikana mahali alipo hadi sasa.
Katika mahojiano na gazeti la The Poughkeepsie Journal, muumini wa kanisa hilo Isis Vermouth alisema jamii itamlaani aliyechoma nyumba yao.
“Kila mtu ameshtuka na wanaoishi karibu wana wasiwasi. Ambaye alitenda kitendo hiki atalaaniwa na kila mmoja wetu. Nahisi kama huu ulikuwa mchezo mchafu,” alisema.
Nyumba hiyo ambayo ilijengwa na Joe Mendilloin miaka ya 1900, imekuwa ikihudumia jamii kwa muda mrefu na hivyo mkasa huo wa moto uliwakasirisha wanachama wengi. Hali ya kanisa hilo kwa sasa itawalazimu jamii kujenga jengo hilo upya.
“Kwa sasa haijulikani ni lini jengo hilo litajengwa kwa sababu ya uharibifu mbaya wa moto,” alieleza Peter Gilmore ambaye ni kuhani mkuu wa kanisa hilo.
Gilmore pia aliongezea kuwa kanisa hilo haliabudu shetani kama ilivyokuwa ikiripotiwa kwa miaka kadhaa na hata kumfanya mmiliki wa awali Mendillo, kujitokeza hadharani na kuwaalika watoto na kuwapa peremende.
Comments