Featured Post
SIRI 10 KAMA MCHUMBA/MPENZI WAKO ANAKUPENDA KWELI
- Get link
- X
- Other Apps
SIRI 10 KAMA MCHUMBA/MPENZI WAKO ANAKUPENDA KWELI
Binadamu wengi tumezungukwa na giza kubwa sana hasa pale inapokuja kwenye swala la mapenzi na wakati huo unakuta umependa kweli, huwa ni ngumu kuelewa yupi mkweli na yupi muongo.
Unapokuja kwenye swala la mapenzi ni lazima uweke utani na mchezo pembeni kwasababu mapenzi yanaweza kukupelekea kifo.
Kiujumla wengi wetu tumesha teseka kwenye mapenzi na inakuwa ngumu sana kumtambua mtu ambaye anakupenda kweli hasa pale wewe unapokuwa umempenda huyo ambaye unahitaji na yeye akupende.
Leo hii nimekuletea siri 10 za kumtambua mchumba au mpenzi anayekupanda kweli wakati unapokuwa kwenye mahusiano.
1.Anakuheshimu na anakufanyia mambo yote kwa heshima
Mchumba anayekupenda lazima ataonyesha heshima kwako hata kama kuna jambo la ajabu utakuwa umelifanya, halitamfanya akudharau bali atakurekebisha kwa kukwambia kwa heshima lakini haitakupunguzia credit za upendo kwako.
2.Mda wote uko kichwani kwake/anakuwaza wewe
Mara nyingi sana hili ni jambo ambalo kama umeshakuwa kwenye mapenzi utakuwa unao uzoefu ni jinsi gani huwa una muwazaga mpenzi wako, mchumba anayekupenda kweli muda wote atakuwa anakuwaza na kama mpo mbali unaweza ukalitambua hilo kwakuwa atakuwa anakutumia sms, kukupigia simu, anakujulia hali kila wakati hata kama mkiwa mnafanya kazi sehemu moja basi atakuwa anapenda sana kukuona na kukufwata kila wakati.
3.Anakusikiliza na anafanya unachokisema
Mapenzi ya kweli yanasindikizwa na heshima, mpenzi anayekupenda kweli huwa haonyeshi kiburi wala kukukunjia mdomo pale unapomwambia jambo Fulani badala yake huwa anakusikiliza na kuheshimu kile unachokisema.Endapo atakuwa hajakubaliana na kile unachokisema, atatumia sauti ya upole kwa kukwambia huku akiweka maneno kama(lakini baby,kwanini tusifanye hivi,ila mi naona,kiukweli mi sijapenda) na njia nyingine nyingi za upendo
4.Anaweza kukushika bila kuogopa watu. mfano, mkono mkiwa sehemu zenye watu wengi
Mchumba anayekupenda kweli ni lazima anakuwa anajiamini na haogopi watu, anaamini wewe ni wake na wakati unafanya kitendo hicho ataonyesha furaha na kukubali kwa kile unachokifanya.
5.Anakujali
Mpenzi anayekupenda kweli hatokuacha uteseke, atakujali kwa kila hali hata kama atakuwa hana fedha basi atajitahidi kutumia hata ushauri wa mawazo, na kama ni jambo ulikuwa unafwatilia,basi atahitaji kujua kama umefanikiwa au la.
6.Anataka uipende na ushirikiane na familia na ndugu zake
Wanasema ukipenda Boga penda na ua lake, mpenzi wa kweli hupenda kuona anayempenda amependa pia upande wa ndugu zake katika familia na hata ndugu wengine waliomzunguka.
7.Anaweza kuomba msamaha
Kwenye mapenzi kuna kukwaruzana na hali hii hupelekea watu kuwa katika hali ya kutoelewana lakini katika hatua hii jambo kubwa ni lazima uangalie uzito wa kosa upo kwa nani na mmoja kati yenu ajishushe kuomba msamaha.Endapo mtakuwa wote vidume humo ndani basi kuna uwezekano kukatokea mtafaruko kwenye mapenzi yake.
8.Akiwa anaongea badala ya kusema nita…. anasema tuta…. mfano, tutafanya hivi badala ya nitafanya hivi.
Usipende kuwa mbaguzi wa mambo, hakikisha kwenye mapenzi kama ukiwa na mwenza wako jua kufanya kila kilicho chako ni cha kwake na chake ni chako, kwahiyo jua kutumia usemi wa tuta,ile gari yetu,ile nyumba yetu, ule mpango wetu na mambo mengine ambayo mnahitaji ushirikiano.
9.Anakuweka kwenye mipango yake ya baadae
Ukitaka kujua mpenzi wako ni wa kweli ni lazima atakuwa na ndoto na wewe na endapo ukisikia ama kuona anakupanga kwenye mipango yake ambayo itakamilika labda miaka 2 au mitano ijayo, jua huyo ndyo chaguo lako pendwa na anakupenda kweli.
10.Anasema ‘SASA’.
(Mfano SASA tufanyeje?) Anatumia neno sasa kukupa nafasi ya kutoa mawazo yako endapo utakuwa unahitaji msaada wa mawazo.Ila chunga sana usije ukakosea ukawa unawaza jambo na kusema sasa nitafanyaje nay eye haujamshirikisha, atagundua kuwa unamdharau na unaona kuwa yeye hana umuhimu wowote kwako kwa hilo jambo unalotaka kufanya ila unashindwa kumwambia.
Comments