Featured Post

5 Things to Do to Secure Your Facebook Account From Hackers

Image
  Some time back, a Facebook account was irrelevant to hackers. There was no reason to hack anyone’s account since there was no reason for hacking an account in the first place. Ever since it has grown to billions of users, Facebook contains enough data for hackers to use for either monetary gain or blackmail. A celebrity’s account, for example, can be hacked in order for a person to advertise a page or brand. The hacker can also post embarrassing or discriminating posts that will leave the celeb’s fans furious. Your account is also prone to hacking even if you aren’t a celebrity. You obviously have to protect your  Facebook account from malicious hackers . It is not that hard to protect your account. Just follow these guidelines, and you’ll be good to go: 1) AVOID SAVING PASSWORDS ON PUBLIC DEVICES Cybercafés are awesome alternatives when you do not have any data on your device. They are also reserves for passwords since most people just click on ‘yes’ on the save password di...

Hawa Nd’o Wanyama 10 Wenye Kasi Zaidi Duniani

 

Hawa Nd’o Wanyama 10 Wenye Kasi Zaidi Duniani

WANYAMA au viumbe wenye kasi zaidi duniani miongoni mwao huruka angani, wengine huogelea baharini na wengine hukimbia ardhini.

 

Kulingana na mtandao wa OneKindPlanet unaoangazia elimu ya wanyama, wanyama wafuatao ndiyo wenye kasi zaidi duniani:

 

 

10. Sungura wa Hudhurungi

Ana miguu mirefu ya rangi nyeusi inayomwezesha kukimbia kwa kasi ya kilomita 77 kwa saa, kasi sawa na mbwa-mwitu mwekundu.

 

 

9. Nyumbu wa Samawati
Nyumbu wa buluu, springbok na gazelle wote wanaweza kukimbia kasi ya kilomita 80 kwa saa karibu sawa na kasi ya simba

 

8. Samaki aina ya Marlin

Marlin anaweza kuogelea kwa kasi ya kilomita 80 kwa saa, akinyang’anywa taji hivi karibuni na samaki aina ya Sail ambaye ndiye mwenye kasi zaidi duniani.

 

7. Paa wa Pembe la Kuchoma
Swala aina ya Pronghorn ni mnyama wa pili wa ardhini mwenye kasi ya kilomita 98 kwa saa.

 

6. Samaki wa Tanga
Samaki huyu ni mwenye kasi zaidi duniani, akiwa na kasi ndani ya maji ya kilomita 110 kwa saa.

 

5.Duma
Duma ana ujuzi katika kukimbia haraka na anaweza kufikia kasi ya kilomita 113 kwa saa.

Hiyo ni kasi kubwa mara tatu ya binadamu ambaye ana uwezo wa kukimbia kilomita takribani 36 kwa saa. Duma wana ujuzi kuliko mnyama mwingine wa aina yake.

 

4. Bata bukini- mwenye mabawa ya ncha
Bata bukini ni bata mkubwa duniani anayeweza kupaa kwa kasi ya kilomita 142 kwa saa.

 

3. Ndege Msindikizaji
Hukimbia umbali wa kilomita 153 kwa saa anasaidiwa na urefu wa mabawa yake ukioanisha na uzito wa mwili wa ndege yeyote. Ndege hawa wana uwezo wa kukaa angani kwa zaidi ya wiki moja.

 

2. Ndege aina ya Spine Tailed Swift
Ni ndege mwenye rangi nyeupe shingoni na mkia uliochongoka, ni ndege mwenye zaidi anapopaa akiwa na kasi ya kilomita 171 kwa saa.

 

1.Kipanga

Ndiye ndege mwenye kasi zaidi, kwa hakika ndiye mnyama aliye na kasi zaidi kwenye sayari, wakati akiwa kwenye mbizi ya uwindaji, huinuka kwa umbali mrefu, kisha huzama kwa kasi ya zaidi ya kilomita 322 kwa saa.

Comments

Popular posts from this blog

14 Tips for Winter Holidays during the COVID-19 Pandemic

COVID-19 Vaccines: Myth Versus Fact

5 Things to Do to Secure Your Facebook Account From Hackers