Featured Post
HABARI:Walimu 2 Mbaroni Wakituhukiwa Kumpa Mimba Mwanafunzi na Kuitoa
- Get link
- X
- Other Apps
POLISI mkoani Njombe inawashikilia walimu wawili wa Shule ya Sekondari Mang’oto wilayani Makete mkoani Njombe, kwa tuhuma za kumsababishia ujauzito na kumtoa mwanafunzi wa shule hiyo mwenye umri wa miaka 17.
Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa, amesema wanamshikilia mwalimu Ezekiel Thomas (36) maarufu kwa jina la Dokole, kwa kuwa na mahusiano na mwananfunzi na kumsababishia ujauzito.
“Huyu mwalimu amekuwa na mahusiano na mtoto wa sekondari mwenye umri wa miaka 17 na binti huyo amepimwa amegundulika ni mjamzito,”alisema Issa.
Aidha amesema wanamshikilia mwalimu Ben Liamdilo (35) kwa kushirikiana katika tukio la utoaji wa mimba na kumsababishia maumivu mwanafunzi huyo.
“Mwalimu Thomas alifanya juhudi akamtuma huyu mwalimu mwenzake akambeba na bodaboda kwenda kumtoa mimba na mpaka sasa hivi walimu wote wawili tunawashikilia na wanatuhumiwa na makosa haya,” alisema Issa. Vile vile ameitaka jamii kushirikiana kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ili kukabiliana na vitendo kama hivyo.
Comments